Maji: Magonjwa, Usafi na Mazingira ni kitabu kinachotoa elimu kwa Watoto na watu wazima kuhusu umuhimu na hatari za maji.Kitabu kinafafanua, kwa lugha nyepesi na inayozoeleka, kuhusu namna tunavyopata magonjwa yatokanayo na maji pamoja na njia za kuyazuia. Kinaonesha wazi kuwa mazingira ya maji ni hali halisi katika maisha ya watu wanaoishi katika nchi zinazoendelea. Kwa hiyo, ni lazima tuwe na stadi za maisha zitakazotuwezewha kuishi maisha yaliyo salama bila magonjwa. Sura saba katika kitabu zinagusia vipengele muhimu vya malengo ya millenia kuhusu maji na mazingira yake, kama ifuatavyo: Sura ya Kwanza: Vyanzo na Matumizi ya Maji Sura ya Pili: Maji Yanaweza Kuwa Hatari Sura ya Tatu: Tabia Hatarishi Katika Matumizi ya Maji na Athari Zake Sura ya Nne: Athari za Mazingira Machafu ya Maji Sura ya Tano: Tulinde Maisha Yetu, Tuwe na Maisha Bora Sura ya Sita: Tujenge Tabia Salama, Tuwe na Stadi za Maisha Sura ya Saba: Uhaba wa Maji na Magonjwa.