Tabia za Sayari Katika Mfumo wa Jua kinafafanua kwa kina zaidi kuhusu sayari Dunia miongoni mwa Sayari nyingine katika Mfumo wa Jua. Tabia muhimu ambazo zinapambanua sayari, ikiwemo Dunia katika Mfumo wa Jua, ni pamoja na: Kuundwa kwa miamba na metali; kuundwa kwa gesi na barafu, sayari kuwa kubwa, pamoja na sayari kuzunguka Jua. Uhusiano wa Jua na sayari Dunia amabao unaipa Dunia tabia za kipekee miongoni mwa Sayari nyingine katika Mfumo wa Jua umefafanuliwa kwa kuelezea matokeo ya Dunia kujizungusha yenyewe wakati inazunguka Jua na pia matokeo ya Dunia kuzunguka Jua. Dhana ya maji kupwa na kujaa kila siku pande tofauti za Dunia inaelezea moja ya uhusiano wa Jua, Dunia na Mwezi na mizunguko yao..