Sayari Katika Mfumo wa Jua, ni kitabu kinachompa maarifa kuhusu anga. Kinazingatia maarifa kuhusu sayari nane zilizo katika mfumo wa Jua. Sayari katika mfumo wa Jua zilitokea na kuwa katika mpangilio maalumu kutoka kwenye Jua kama ifuatavyo: Zebaki ni sayari ya kwanza kutoka kwenye Jua, inafuatiwa na Zuhura, Dunia, Mirihi, Sumbula, Sarateni, Zohari na Kausi, ambayo ni ya mwisho. Ukanda wa Asteroidi unatenganisha sayari zenye uso mgumu na zile zenye uso wa gesi na barafu. Pia, katika sayari za mfumo wa Jua, ni sayari Dunia pekee ndipo viumbehai wanaishi juu ya uso wake. Mwanga asili wa Jua umekuwa na manufaa makubwa kwa sayari Dunia na Viumbehai vyote vinavyoishi juu ya uso wake. Mwanga wa jua umewezesha binadamu kuishi kwa mafanikio makubwa juu ya uso wa sayari Dunia..