Wacha Mungu wa Bibi Kiliona

TSH 20000.00 /=
Author:Gabriel Ruhumbika
Year Published: 2014
ISBN:9789987735112

Wacha Mungu wa Bibi Kiliona ni riwaya inayotumia utafiti mkubwa na yakinifu kutupia mwanga historia ya jamii ya mtanzania na Mwafrika tangu na kabla ya ukoloni hadi leo hii.Mateso ya mtu mweusi kwenye historia yake mapambano yake,shida,mafanikio na matumaini yake tangu ajitawale,ndiyo maudhui ya hadithi ya Bibi Kilihona na WachaMungu” wake wawakilishi wanne na wajukuu wake wengi wa kiladini,rangi,taifa na kabila,mithili ya jamii ya leo ya Watanzania na Waafrika wote. Baada ya Bibi Kilihona kufariki mwaka wa 1995,akiwa na umri wa miaka 113,aliwatokea“WachaMungu”wake na kuwataka waanzishe dini mpya zitakazowaelekeza waumini wa dini zote nchini kuishi kwa pamoja kwa amani na kupendana na kuheshimiana.Aliwaambia “Wacha Mungu wa dini zote na wana wapenzi wa Mungu Muumba wetu sote”Walipoanzisha hizo dini wakauawa wote na magaidi! Hadithi hii ya kihistoria ya kusisimua inamtaka msomaji wa Kiafrika ayafikirie upya na kwa makini mambo mengi muhimu kwenye maisha yake na ya jamii yake ambayo hayaendi sawa,kubwa kati yake likiwa ni dini yake kwenye nchi yenye dini nyingi na katika dunia ya leo.Pia,hadithi inawatukuza “bibi na mama wote wa Mwafrika’’kwa hekima na utu-mwema mkubwa wa Bibi Kilihona licha ya maovu aliyotendewa maishani mwake! Niseme tu Kwamba nimevutiwa sana na riwaya hii,na binafsi ningefurahi kama ingesomwa na kila mwafrika anayeweza kusoma,na ingetafsiriwa katika lugha nyingi,na kusomwa katika shule zote”.

Similar Fiction Books

Sale product image

Parched Earth

TSH: 1200.00

Sale product image
Sale product image

Marimba ya Majaliwa

TSH: 12000.00

Sale product image

Run Free

TSH: 10000.00

Sale product image

Mwendo

TSH: 10000.00

Sale product image

The Prisoner

TSH: 10000.00

Sale product image

Pambazuko Gizani

TSH: 7000.00

Sale product image

Mpe Maneno Yake

TSH: 10000.00

Sale product image

Nuru ya Bhoke

TSH: 10000.00

Sale product image
Sale product image