Madhila ya Faidha ni hadithi ya kusimumua kwa vijana inayoweka mkazo juu ya kupinga unyanyapaa na ukatili unaofanyika dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi,albino.Faidha amezaliwa na ulemavu wa ngozi na amekuzwa katika familia yenye upendo na msimmo.Wazazi wake faidha walitafuta ukweli juu ya ualbino kwa wataalum ili waweze kumtunza Faidha vizuri na kuieliemsha jamii inayowazunguka.Pia walitaka kujua ni kwa nini wazazi ambao sio albino wanaweza kuzaa mtoto albino. Wazazi wa Faidha wanafanikiwa.Faidha anafanya vizuri katika masomo na ana kipaji cha uchoraji ambacho kinailetea shule sifa.Katika maisha ya kila siku,Faidha anakumbana na vikwazo vingi na wakati mwingine maisha yake yanakuwa hatarini. Fuatilia kisa hiki..