SITASAHAU MV BUKOBA ni kitabu kinachoelezea hali halisi ilivyokuwa ndani ya meli ya Mv Bukoba kabla na baada ya ajali.Nyaisa Simango ni miongoni mwa abiria wachache tu walionusurika katika ajali hiyo.Anajaribu kuelezea tangu mwanzo wa safari yake toka Dar es Salaam kwa treni hadi Mwanza na kutoka Mwanza kwenda Bukoba na safari yake kurudi kutoka Bukoba na meli hiyohiyo hadi ilipoishia kwa kupinduka na kuzama,kiasi cha maili kumi hivi kabla ya kufika bandarini Mwanza.Amejaribu kuelezea matatizo mbalimbali ya MV Bukoba tangu mwanzo wa safari hadi kuzama kwakwe,na atahari za ajali hii kijamii,kiuchumi na kisiasa.Mwisho anahitimisha kwa kutoa uchambuzi wa majanga kama haya,mapendekezo na ushauri kwa taasisi mbalimbali zinazotoa huduma kwa jamii..