Mlima Kilimanjaro Ni fahari ya Tanzania. Ni mrefu kuliko milima yote katika bara la Afrika Ni miongoni mwa milima mirefu duniani inayosimama peke yake. Mlima Kilimanjaro,Fahari Yetu kinaelezea umuhimu kuhusu Mlima Kilimanjaro.Kwa kutumia taarifa za wanasayansi watafiti waliochunguza barafuto za milima mikubwa duniani kwa muda mrefu,kitabu kinatoa maelezo ya kina kuhusu ni kwa nini barafuto za Mlima Kilimanjaro zinapotea kwa kasi,kinaelezea pia faida za mlima kwa jamii inayouzunguka na taifa kwa ujumla,pamoja na wajibu wetu katika kuhifadhi mazingira ya Mlima Kilimanjaro ambao ni urithi wa Watanzania wote..