Sale

Daraja Juu ya Mto Nile

TSH 30000.00 /=
Author:Mark Mwandosya
Year Published: 2000
ISBN:9789987735389
Availability: 9 left in stock

Mto Nile ni mrefu kuliko mito yote duniani,ambao katika historia umekuwa chimbuko la mshangao,udadisi,utafiti,uchunguzi na chanzo na makutano ya ustaarabu,biashara,himaya mbalimbali, sayansi na teknolojia na uhandisi. Mto Nile na Bonde lake unaunganisha nchi 11 ambazo ni Burundi, Eritrea, Ethiopia, Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo,Kenya,Misri,Rwanda,Sudan ,Sudani ya kusini,Tanzania na Uganda.Sehemu ndogo ya Bonde la Nile iko Jamhuri ya Afrika ya Kati. Kitabu hiki,DARAJA JUU YA MTO NILE,kinachambua jiografia,uhandisi,siasa na juhudi za ushirikiano kati na baina ya nchi za Bonde hilo.Watafiti wa masuala ya majishirikishi na wanasiasa wametabiri kwamba vita zijazo duniani zinatokana na kutokuelewana katika matumizi ya maji.Mwandishi Prof.Mwandosya, anaamini kwamba Mto Nile unaweza na utakuwa daraja la ushirikiano na umoja baina ya nchi za bonde hilo.Imani hiyo inatokana na juhudi za nchi hizo miaka mingi zilizofanikisha kupatikana kwa mkataba Mhimili wa ushirikiano baina Nchi za Bonde(Nile Basin Cooperative Framework Agreement-CFA).Chimbuko la kitabu hiki ni uzoefu alioupata mwandishi,kama mtendaji ndani ya serikali,mwalimu na katika majadiliano yaliyofanikisha kupatikana kwa CFA. DARAJA JUU YA MTO NILE ni kitabu kinachovuta utashi wa kutaka kuelewa undani wa mazingira ya maji na siasa zake.Kitabu hiki kitakuwa na faida kubwa hasa kwa wanafunzi,wasomi,watafiti wa masuala ya majshirikishi na wanasiasa. Kuhusu Mwandishi Mark James Mwandosya ni mhandisi mwandamizi,mwandishi wa vitabu vya uhandisi,mazingira,mabadiliko ya tabianchi na matumizi ya rasimali za maji.Prof Mwandosya ni mwalimu aliyefundisha kwa miaka mingi katika chuo kikuu cha Dar es Salaam, Tanzania. Amewahi kuwa kamishna wa masuala ya Nishati na Petroli; Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji,Nishati na Madini;Katibu Mkuu Wizara ya ya Viwanda na Biashara;Waziri wa mawasiliano na uchukuzi:Waziri wa Mazingira;Waziri wa Maji na Umwagiliaji;Waziri wa Maji ;na sasa ni Waziri wa Nchi,Ofisi ya Raisi na Mbunge wa Rungwe Mashariki, Tanzania..

Similar Books

Sale -11% product image

Batin crofessor pampden

$110.00$130.00

Sale -11% product image

Batin crofessor pampden

$110.00$130.00

Sale -11% product image

Batin crofessor pampden

$110.00$130.00

Sale -11% product image

Batin crofessor pampden

$110.00$130.00

Sale -11% product image

Batin crofessor pampden

$110.00$130.00