Udhibiti ni njia mojawapo inayotumika kusimamia Uchumi wa nchi na kuendeleza ustawi wa jamii.Udhibiti wa huduma za kiuchumi (public utilities) unahusu kuweka mizania kati ya kuwawezesha watoa huduma na kuwalinda watumiaji wa huduma kama vile maji, umeme, uchukuzi, mawasiliano na utangazaji. Kitabu hiki kinaelezea chimbuko la udhibiti Tanzania katika muktadha wa mabadiliko ya uchumi duniani pamoja na udhibiti katika nchi nyingine.Ni kitabu chenye maarifa ya msingi kwa kila mtumiaji wa huduma za kiuchumi,pamoja na wanafunzi,wasomi, wafanyakazi na viongozi. Kuhusu Mwandishi Mwandishi wa kitabu hiki,Mark Mwandosya, amewahi kuwa Profesa wa Uhandisi Umeme Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,Kamishna wa Nishati na masuala ya Petroli,Katibu Mkuu Wizara ya Maji,Nishati na Madini,Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara,Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi,Waziri wa Nchi (Mazingira),Ofisi ya Makamu wa Rais,Waziri wa Maji na Umwagiliaji,na Waziri wa Maji.Kwa sasa yeye ni Waziri wa Nchi(Kazi Maalum),Ofisi ya Rais. Katika nafasi mbalimbali amesimamia kuanzishwa kwa mamlaka za udhibiti wa Uchumi Tanzania..