Rafiki Mpenzi Hamiata Je hujambo? Mambo ya huku Mtwara ni Mengi mno. Siwezi kukueleza yote kwenye barua hii.Halafu niliandika kwa Haraka shangazi asije akanikamata.Karatasi yenyewe nimeichomoa kwenye daftari la watu.Sasa sikiliza kwanza. Usiwe na wasiwasi. Yale madhara yaliyomtokea msichana wa Moshi Vijijini hayatanitokea mimi,kwa hiyo tuliza roho yako mpenzi.Shangazi kaniambia kwamba kutahiri mtoto wa kike ni kuvunja nguvu hizo na kuzinyima uhuru.Kwa hiyo shangazi kasema kwamba ni lazima sisi wasichana tukatae katu kufanyiwa hivyo.He! rafiki,nitakueleza mengi tutakapoonana. Wako Rafiki akupendaye sana Felisia..