Mwandishi kwenye Kitabu hiki, UTAWALA BORA, anafafanua, pamoja na mambo mengine, dhana ya Utawala Bora, ile ya Utawala wa Sheria, na mfumo wa Demokrasia; maovu na mapungufu makuu katika nchi nyingi duniani, yakiwemo udhalimu, rushwa na elimi duni; şifa kuu ambazo viongozi katika nchi ya kidemokrasia wanatakiwa kuwa nazo; haki ya usawa wa kijinsia; na yale mambo yanayotakiwa kuwemo katika Katiba Bora ya Nchi. Kwa heshima, msomaji anakaribishwa kuchota elimu kwenye kisima hiki..