Miaka kama millioni mia mbili Dinosaria wa aina mbalimbali wadogo na wakubwa waliishi Tendaguru. Dinosaria hao walitoweka kabisa kutoka Tendaguru miaka milioni sitini na tano iliyopita. Janga la mafuriko linapotokea, viumbe hufunikwa na udongo. Masalia ya viumbe hao yakikaa ardhini kwa muda mrefu huwa magumu kama mawe. Baadaye, mmonyoko wa udongo unapotokea hufukua masalia hayo na kuyafanya yaonekane nje ya ardhi.Kitabu hiki kinasimulia Historia ya Dinosaria wa Tendaguru..