World Wide Fund for Nature(WWF) ni shirika lisilo la kiserikali la hifadhi ya mazingira lililo kubwa kuliko mashirika ya hifadhi yote duniani. WWF ina mtandao wa mashirika 25 ya kitaifa katika nchi mbalimbali, mashirika 6 na ofisi za programmu 22. Lengo la WWF kwa ujumla ni kupunguza na ikiwezekana kudhibiti kabisa kasi ya uharibifu wa mazingira hapa duniani, ili kuboresha maisha ya binadamnu na viumbe wengine katika mazingira yao. WWF Tanzania inajihusisha na: Kuimarisha shughuli za mazingira. Kuhifadhi wanyama na mimea iliyo katika hatari ya kutoweka Kujenga na kuimarisha uwezo wa taasisi zinazohusika na hifadhi ya mazingira. Kutoa Elimu ya mazingira. Kuhimiza ushirikishwaji wa jumuiya nzima katika hifadhi ya mazingira..