Utawala Bora, Vita Dhidi ya Udhalimu,Rushwa na Elimu Duni

TSH 0.00 /=
Author:Jaji Barnabas Albert Samatta
Year Published: 2023
ISBN:9789987735952

Jaji Mkuu mstaafu Barnabas Albert Samatta, mwandishi wa Kitabu hiki UTAWALA BORA, alipata kuwa Mkurugenzi wa Mashtaka hapa Tanzania na Jaji wa Mahakama Kuu huko Zimbabwe, kabla ya kuwa Jaji Kiongozi hapa nchini. Baada ya kustaafu kwenye cheo cha Jaji Mkuu, aliteuliwa kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, na baadaye alipata kufanya kazi nchini Kenya kwa miaka mitatu kama Mjumbe wa Bodi ya Kupima Majaji na Mahakimu (Judges and Magistrates Vetting Board) iliyokuwa na mamlaka ya kuwachunguza Majaji na Mahakimu nchini huko ili kugundua kama walikuwa na viwango vya kuridhisha vya uwezo kazini, uadilifu, uwajibikaji, uhuru na ujasiri kuwawezesha kuendelea kushika vyeo hivyo. Kwa miaka ipatayo mitatu alikuwa, vile vile, Mjumbe wa Bodi ya Taasisi ya Katiba ya huko huko Kenya (Katiba Institute of Kenya). Kwa wakati huu, yeye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Kituo cha Sheria na Haki Za Binadamu (Legal and Human Rights Centre) cha hapa Tanzania. Ni mwandishi wa vitabu kadhaa, kikiwemo SUPREMACY OF LAW (UKUU WA SHERIA). Kwenye Kitabu hiki, UTAWALA BORA, anafafanua, pamoja na mambo mengine, dhana ya Utawala Bora, ile ya Utawala wa Sheria, na mfumo wa Demokrasia; maovu na mapungufu makuu katika nchi nyingi duniani, yakiwemo udhalimu, rushwa na elimu duni; sifa kuu ambazo viongozi katika nchi ya kidemokrasia wanatakiwa kuwa nazo; haki ya usawa wa kijinsia; na yale mambo yanayotakiwa kuwemo katika Katiba Bora ya nchi. Kwa heshima, msomaji anakaribishwa kuchota elimu kwenye kisima hiki..