Tamati Tamthilia

TSH 0.00 /=
Author:TANZANIA GENDER NETWORK PROGRAMME
Year Published: 2021
ISBN:978997656691

Tamthiliya hii ya TAMATI inaakisi mgongano uliopo kati ya mitizamo ili ndani ya jamii kuhusu maisha ya mtoto wa kike wakati huu wa karne ya 21, ambapo mafanikio katika maisha yanategemea kupata maarifa na elimu. Mtizamo mmoja unazingatia uhuru, utu na matamanio ya mtoto wa kike, ambao unaoneshwa na msichana mpambanaji Ghati katika tamthiliya, na ambao ndio pia msimamo wa viongozi na jamii husani wanawake wapenda maendeleo, Mtazamo mwingine ni ule ulioganda katika kunyanyasa,kudharau na kuonea watoto wa kike kwa kuwakeketa, kuwanyima elimu na kuwaoza katika umri mdogo,ukielezwa kuwa ni mila na desturi ambazo zilitawala karne zilizopita. Tamthiliya inatambua umuhimu wa utamaduni katika maisha ya binadamu, na kuna waumini wake wanaosema, "ni lazima tuwe watu wanaoelekea mbele,sio kutazamatazama nyuma na kutamani kurudi,...... tubebe yaliyo mema tuende nayo mbele....".