Tufurahie Namba 1: Tujue Kuhesabu ni kitabu cha kwanza katika mfululizo wa vitabu kumi. Vitabu hivi vimeweka mkazo katika kutoa elimu ya namba kuanzia ngazi ya chini ya chekechea hadi ngazi ya juu inayolenga watoto wa darasa la sita na la saba. Kitabu hiki cha kwanza kinamsaidia mtoto anayeanza kuhesabu 1 hadi 10. Mazoezi mepesi yametolewa ili kumwezesha mtoto mwenyewe, mzazi au mwalimu, kuhakikisha kwamba mtoto ameelewa namba hizo vizuri. Ngazi: Chekechea na darasa la Kwanza..