Wanawake wa TANU Jinsia na Utamaduni katika Kujenga Uzalendo Tanganyika: 1955-1965

TSH 0.00 /=
Author:Suzan Geiger,TGNP
Year Published: 2005
ISBN:9987600115

Wananchi wa Tanganyika walijipatia uhuru wao kutoka kwa Waingereza mwaka 1961 kupitia mapambano yaliyoongozwa na jumuiya yenye nguvu chini ya uratibu wa chama cha TANU. Wanawake wazalendo walikuwa ni viongozi mashuhuri katika medani zote kwenye ngazi mbalimbali. Kiatbu hiki kinauliza maswali kadhaa: Ni kwa nini utaifa wa Mtanzania ulichukua sura mpya baada ya uhuru kuliko ilivyokuwa katika nchi nyingine? Je, tunauelezeaje ukweli kwamba licha ya tabia, utaifa wa Tanganyika umebaki kuwa alama tu ya utambulisho kwa wanawake? Je, ukiangalia ukweli kuwa utaifa na utamaduni katika Tanganyika vilikuwa kazi zilizoendeshwa na wanawake wa TANU, matokeo ya kazi yao ni yapi? Je, tunauelezeaje ukweli kuwa utaifa hapa Tanzania haukujengwa na kikundi cha wanamapinduzi au haukuwa ni matokeo ya kuibuka kwa matabaka kutaka kudhibiti dola?.