Simulizi za Bui bui ni mfululizo wa Viitabu vya maarifa kwa watoto wa ngazi za chini.Vitabu hivi vinalenga wasomaji ambao wanajua kusoma kwa ufasaha kuanzia darasa la pili na kuendelea. Mfululizo huu unahusu viumbe wadogo katika maisha ya kila siku ya mtoto .Viumbe hawa wanaishi katika mazingira ya Nyumbani yanayomzunguka Mtoto. Madhumuni ni kujenga Tabia za kisayansi kwa watoto tangu mapema.Vitabu vinalenga kuamsha na kuchochea udadisi.Pia vinalenga tabia na ari ya uchunguzi katika mazingira..