Atlasi ya TANZANIA ya Ujifunzaji Shirikishi kwa Shule za Msingi Atlasi hii ya Tanzania ya Ujifunzaji Shirikishi inasisitiza kwenye mahitaji mahususi kwa wanafunzi na waalimu wa Shule za Msingi za Tanzania.Atlasi inatoa taarifa kwa upana na kinaganaga kuzingatia Muhtasari Mpya wa Jiografia kwa Darasa la 3 mpaka la 7. Atlasi ya Ujifunzaji Shirikishi ina tofauti ya pekee kwa sababu inampa mwanafunzi ufafanuzi unaohitajika kuhusu dhana muhimu za ramani:pamoja na shughuli nyingi ambazo zimewasilishwa katika viwango mbalimbali kwa kila darasa kulingana na ugumu wa maudhui yaliyomo kwenye Muhtasari. Kwa njia hii Atlasi ya Ujifunzaji Shirikishi inatoa nafasi kwa mwalimu na mwanafunzi kukazana kufanya mazoezi muhimu na ya lazima ya stadi za ramani,pamoja na umakinifu,ufumbuzi wa matatizo/maswali na stadi za uchunguzi Ili kuimarisha zaidi stadi za ramani na kuboresha ujifunzaji shirikishi kwa waalimu na wanafunzi,Atlasi hii ni ya pekee kwenye soko la vitabu vya elimu Tanzania,kwani inaambatana na Kiongozi cha Mwalimu Kiongozi hiki kinampa mwalimu yafuatayo: Mwongozo wa’ jinsi ya’ katika kufundisha stadi za ramani,kama vile jinsi ya kutengeneza vifani,jinsi ya kutumia na kujifunza kwa picha,jinsi ya kuchora na kusoma ramani na jinsi ya kufundisha kwa kutumia Atlasi. Usuli wa umuhimu wa stadi za ramani na jinsi ya kutumia Atlasi(na ramani kwa ujumla) katika ufundishaji. Andalio la somo,pamoja na mapendekezo mengine,ili waalimu waweze kuwasaidia wanafunzi kukuza stadi za ramani. Majibu kwa mazoezi yaliyomo kwenye Atlasi na vidokezo vya jinsi ya kufanya mazoezi. Vipengele vingine muhimu na vya kuzingatia vya Atlasi ya Ujifunzaji Shirikishi vinajumuisha yafuatayo: Wingi wa maelezo yaliyoonyeshwa kwenye ramani yemechaguliwa kwa uangalifui ili kukidhi mahitaji mahususi ya mwanafunzi na waalimu wa shule ya msingi. Taarifa ambazo ni za wakati huu ndizo zimetumika kutengenezea ramani na picha nzuri, za kuvutia na kufaa kufuatana na mahitaji ya mutasari. Maudhui ya Atlasi yameonyeshwa wazi kwa rangi na ukurasa mwanzoni mwa Atlasi ili iwe rahisi kutumia.Kurasa zote za Atlasi zina rangi pia. Faharasa rahisi ya majina ya sehemu muhimu kwenye Atlasi imetolewa pamoja na maelezo ya jinsi ya kutumia Faharasa hiyo..