Ijue Biashara: Hesabu za Biashara

TSH 700.00 /=
Author:Aleerwa N. Lema
Year Published: 2010
ISBN:9789987735623

Tutafakari misemo hii ya kiswahili: Mali bila daftari hupotea bila habari. Biashara ni asubuhi hesabu jioni. Hii misemo miwili inatukumbusha na kutusihi kuweka kumbukumbu za maamala za biashara,na kisha kuzitafakari baada ya muda.Hivyo,ni vema hesabu za biashara zikawekwa kwa namna ambayo mwenye biashara au mtu mwingine yeyote ataweza kuzipata wakati wowote atakapozihitaji. Umuhimu wa Kuweka mahesabu ya Biashara ni: i.Mwenye biashara atahitaji kujua faida ya biashara yake,na hii faida haipatikanai kwa siku moja. ii.Mwenye biashara atahitaji kujua kama biashara yake inakua ama inadumaa au inakufa.Kukua au kufa kwa biashara hakutokei siku moja,bali ni mwenendo wa biashara wa siku nyingi. iii.Wadau wa biashara nao wangependa kuona kwamba haja zao zinatimizwa kwa siku moja..

Similar Business Books